Maelekezo kwa jamii
-
Kupanua mawazo
Jukwaa la mtatndaoni limekusudiwa kuleta mawazo chanya ili kuboresha mitazamo yetu. Weka au tuma habari ambazo zitaamsha fikra za kila mmoja wetu katika kufikia malengo yetu tuliyojipangia
-
Kujifunza
Kusudi la jukwaa hili ni kutoa mafunzo mbalimbali kwa jamii. Toa mchango wako na rasilimali zako ambazo zinaweza kusaidia kuongeza ustawi wa jamii na maarifa. Kumbuka kutoa pongezi kwa mchango mzuri wa mawazo ya wenzako
-
Msaada
Shiriki katika mijadala yenye kuwatia moyo wengine na kujenga. Usiweke mawazo au mchango wako ambao utawavunja moyo wengine au wenye taswira mbaya.
-
Heshimu
Sisi ni sehemu ya jamii pana duniani hivyo sehemu hii ni muafaka katika kupata mawazo na mitazamo tofauti. Usiweke au usirushe habari ambazo zinaharibu utu wa mtu, au kundi, au rangi ya mtu, au kabila, au ulemavu, au jinsia, au umri au mtazamo wa kihisia za kimapenzi.
-
Taaluma
Mahali hapa pamewekwa mahususi kwa ajili ya kusaidia ajira kwa vijana na kujikimu. Usiweke au kuhusisha lugha mbaya, au vitu vvyenye taswira mbaya au vinavyoshwawishi uvunjifu wa sharia.
Kama unajambo lolote kuhusiana na matumizi sahihi ya mahali hapa au ungependa kutoa taarifa juu ya matumizi yasiyofaa, unashauriwa kutoa taarifa kwa Meneja wa Mafunzo na Taaluma aliyeko katika kituo chako cha EQWIP HUB au kwa barua pepe eqwiphubs@takingitglobal.org